GET /api/v0.1/hansard/entries/1201411/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201411,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201411/?format=api",
    "text_counter": 491,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Usafiri wa ndege; kwa watalii wa humu nchini, umekuwa ghali kwa sababu Kenya Airways ambalo ndilo shirika la ndege linalofanya biashara katika eneo la Mombasa, Kisumu na kwingineko linadai gharama kubwa kuliko wengine wote. Kwa mfano, tikiti ya economy leo kutoka Mombasa kuja Nairobi asubuhi iliikuwa shilling elfu thelathini. Hiyo ni karibu dola mia tatu ambazo zinaweza kukupeleka kutoka Mombasa hadi London ama Frankfurt kwa ndege zinazotoka nje."
}