GET /api/v0.1/hansard/entries/1201415/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201415,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201415/?format=api",
    "text_counter": 495,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Pili, Uchumi Samawati ni jambo ambalo halikutajwa katika hotuba ya Rais, lakini ni muhimu sana kufufua uchumi wa Kaunti za pwani. Tunao ufuo wa bahari kutoka Lungalunga ama Vanga kusini mpaka Kiunga kaskazini. Sisi kama wenyeji wa eneo lile hatujaweza kupata faida zake kamilifu. Kwa mfano, uvuvi wetu bado ni ule wa kiasili. Unavua kutumia vidau, mshipi moja ama nyavu ndogo ambao hausaidii kupata samaki wa kutosha kukuwezesha kulisha familia na kuuza ili kupata mapato ya kukusaidia na familia yako."
}