GET /api/v0.1/hansard/entries/1201417/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201417,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201417/?format=api",
"text_counter": 497,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Katika swala la sheria yani ‘ rule of law’, kuna dalili zinazoonyesha kua serikali hii haitaweza kuheshima uhuru wa sheria. Jambo la kwanza ambalo tuemona ni kuwa mahakama imerushiwa vishawishi kadhaa ambavyo vinavyonyesha kwamba serikali hii iko tayari kuhujumu uhuru wa mahakama. Kwa mfano, siku ya pili alipochaguliwa Rais Ruto, tuliona mambo ya kuapishwa harakaharaka kwa majaji sita yalifanywa haraka ambao walikuwa wamezuiliwa siku za awali. Tumeona pia kuna mipango ya kuongeza ruzuku kwa mahakama kwa jumla. Bw. Spika wa Muda, mwisho ni kuwa Rais alipowasili, jambo la kusikitisha ni kuwa Jaji Mkuu na Naibu wake walikuwa wamesimama kwa msitari hapo nje kumpokea Rais. Hili sio jambo la kawaida. Hata wewe nyumbani kwako, huwezi kualika wageni halafu wageni wa kwanza wakishaingia, unawachukua waandamane na wewe mwenyeji kwenda kuwapokea wageni wengine. Mgeni wako ni wako, mpokee wewe binafsi. Ilikuwa makosa Bunge letu kuwasimamisha wakuu wa Taasisi huru katika nchini, kulingana na kanuni za kumpokea Rais. Mwaka uliopita, kulikuwa na mjadala kuhusu watu fulani ambao walikuwa wamechaguliwa katika nyadhifa za uongozi. Wengine wao walikuwa na tashwishi huku wakiwa wameshitakiwa mahakamani kwa ufisadi na jinai. Waliombwa wajiondoe katika nyadhifa zao kwa muda, hadi makosa yao yathibitishwe ama yaondolewe. Mjadala huo umebadilika sasa. Sasa imekuwa ya kwamba, watu wanachaguliwa kuchukua nyadhifa Serikalini ilihali bado wako na kesi mahakamani. Hii sio dalili nzuri."
}