GET /api/v0.1/hansard/entries/1201419/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201419,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201419/?format=api",
"text_counter": 499,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Inamaanisha tumeanza kupuuza polepole Sura ya Sita ya Katiba inayohusu maadili. Hivi vigezo viwili vinaonyesha kwamba haki haitakuwa inatendeka katika nchi yetu. Katika Bunge la Seneti, tumeona Upande wa Wachache umehujumiwa. Maseneta waliochaguliwa kutoka sehemu hizo wametekwa. Hii sio dalili nzuri katika maswala ya uhuru wa mahakama, taasisi huru kama vile Bunge na pia tume huru za kutetea haki za binadamu. Jambo la mwiso ambalo ningependa kugusia ni maswala ya mbegu zilizobadiliswa na kuweza kuzaa kwa wingi. Kwa Kiingereza tunaita GeneticallyModified Organisms (GMO). Ni hatari kwa nchi yetu kukubali mbegu hizi. Mfano ni hivi majuzi tu ambapo kina dada walianza mtindo wa kudungwa dawa za kuongeza makalio yakuwe makubwa. Hili limeleta hatari kwa wanadada wengi. Juzi katika vyombo vya habari, tumemwona mwana mitindo, Vera Sidika, akizungumzia kuhusu matibabu aliyopitia ili kurekebisha makalio yake. Bw. Spika wa Muda, maswala ya GMO ni kama hivyo. Hatutakuwa na uhakika wa mbegu ambazo sasa tutakuwa tunakula. Hatujui zitaathiri miili yetu kwa njia gani. Tumeshuhudia mkurupuko wa visa vya kansa, maradhi yasiyo na tiba na maradhi mengine ambayo hayaeleweki. Kwa hivyo, hatujafikia kiwango cha kupokea vyakula vya GMO . Hatuna sheria ama kanuni nzuri ambazo zinaweza kudhibiti maswala ya vyakula hivi. Afadhali tubaki na njaa yetu, kuliko kula hivi vyakula vya GMO ambavyo vitatusababishia madhara zaidi. Kwa mfano, mara nyingi hapa Kaunti ya Kitui, watu wamekula mahindi yenye sumu ya ukoga wa mwani au aflatoxin . Ukila sumu aina hiyo, itakudhuru na hata unaweza kufariki. Kwa sasa, hatuna sheria ama kanuni za kudhibiti vyakula hivi. Kwa hivyo, sio salama kwa wananchi wetu kuruhusiwa kula hivyo vyakula. Sisi ni watu wa Upande wa Upinzani na tuko tayari kupambana na maswala ambayo Serikali italeta katika Bunge hili. Ikiwa ni maswala mazuri, tutayaunga mkono lakini ikiwa yataathiri vibaya umma ama wananchi wetu, tuko tayari kuyapinga na kuhakikisha haki imetendeka."
}