GET /api/v0.1/hansard/entries/1201437/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201437,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201437/?format=api",
    "text_counter": 517,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Githuku",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13595,
        "legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
        "slug": "kamau-joseph-githuku"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ningependa kwanza kabisa kuchukuwa nafasi hii kushukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu ya kunijalia kuhudumu katika Bunge hili la Seneti. Vile, ningependa kuchukua nafasi hii kushukuru sana watu wangu wa Kaunti ya Lamu. Hii ni kwa sababu waliona ni vyema, kupitia kwa njia ya kidemocracia ambayo ilifanyika tarehe 09.08.2022, kunipatia fursa ya kuja hapa katika Bunge la Seneti ambalo limeweza kutikwa majukumu ya kikatiba ya kulinda ugatuzi pamoja na serikali zake kama vile ambavyo ilivyonakiliwa katika Kipengele cha 96 cha Katiba ya Jamhuri ya Kenya. Bw. Spika wa Muda, ningependa kuchukua nafasi hii kusema kwamba niliskiliza sana hotuba ya Mhe. Rais. Kati ya mambo aliguzia zaidi ni kilimo, uvuvi na pia ufugaji. Hivo vitengo vyote ambavyo vinahusiana zaidi na ukuzi wa uchumi wa Jamhuri ya Kenya, viko katika Kaunti yangu ya Lamu. Bw. Spika wa Muda, kama vile nimesema vitengo hivi ni muhimu sana katika ukuzi wa uchumi wa Jamhuri ya Kenya. Ukulima ni jambo ambalo limeweza kubaki nyuma katika Kaunti yangu ya Lamu. Ikizingatiwa ya kwamba Lamu ni mahali ambapo pameweza kuwa na shida za kiusalama. Wakulima ambao wako pale ni watu ambao kwa muda mrefu, wameishi wakiwa wamesahaulika sana. Diposa ninachukuwa nafasi hii na kusema kwamba naungana na Seneta wa Kaunti ya Kirinyanga ambaye alisimama hapa na kusema kwamba kuna sheria ambazo ni za ukandamizi ambazo zimeweza kupitishwa na Bunge ambazo zimepita ya kusema kwamba vitu kama vile ufuta, ambao unalimwa kule Lamu, bixa na vile korosho hazitaweza kusafirishwa moja kwa moja kabla hazijakuwa processed katika Jamhuri yetu ya Kenya. Bw. Spika wa Muda, jambo hilo limegandamiza wakulima wetu sana. Ikizaingatiwa pia vile kuna mimea kama avocado ambazo pia zinatakikana kutolewa hapa nchini na kwenda nje ili soko ambayo ni muhimu sana kwa wakulima wetu iweze kuimarika. Bw. Spika wa Muda, Mhe. Rais hakutaja zaidi vile ambavyo atakavyolinda wakulima ambao kwa sasa, wamekuwa katika hali ya utata. Katika mambo ya kuona kwamba mazao yao yameweza kutiliwa maanani. Kupitia kwa jambo hilo, ningependa Bunge hili la Seneti liweze kubadilisha msimamo huo ambao unasema kwamba mazao yetu lazima kwanza iwe processed hapa nchini kabla ya kusafirishwa kuenda nje. Ukiangalia uzalizaji wa nchi hii, shida kubwa ni kwamba mahitaji ni mengi kuliko uzalizaji. Hiyo inasababisha zaidi mazao yetu kukosa bei. Ningehitaji sana kama tungeweza kutengeneza sheria ambazo zitaruhusu moja kwa moja mazao ambayo hayajakuwa processed pia iweze kupata nafasi ya kuenda nchi za nje, kama vile korosho, bixa na simsim ili wale ambao wenatoka sehemu za Asia, waweze kuja hapa kununua mazao hayo na walete ushindani. Kwa kimombo tunaita lawof supply and demand. Sheria hii ifuatwe kwa njia inayostahili ilituweze kulinda mazao ya watu wetu. Bw. Spika wa Muda, jambo la ufugaji litiliwe mkazo zaidi. Hotuba ya Rais ilinakili kwamba ataangalia mambo ya ufugaji. Mifugo inakufa sana kwa wale tunaotoka sehemu kame. Wananchi hawana nafasi ya kuona biashara yao ikinawiri na wanapata hasara kubwa."
}