GET /api/v0.1/hansard/entries/1201439/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201439,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201439/?format=api",
    "text_counter": 519,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Githuku",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13595,
        "legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
        "slug": "kamau-joseph-githuku"
    },
    "content": "Tungependa kupitisha sheria ambapo Serikali itatenga pesa za kununua mifugo wakati wa ukame ili wakulima na wafugaji wasaidike na maisha yao kuendelea. Jambo la uvuvi linaguzia sana kaunti yangu ya Lamu. Kuna miradi mikubwa sana katika Jamhuri ya Kenya kama vile Lamu Port, South Sudan, Ethiopia Transport Corridor (LAPSET). Mradi huu uliwahamisha kwa lazima wavuvi katika sehemu za Lamu. Wakati huu wavuvi wa Lamu wanakosa nafasi za kuvua kwa njia inayostahili. Tulikuwa na mipangilio hapo awali ili watu hawo waweze kufidiwa. Mpaka sasa, hakuna fidia ambayo imeweza kufanywa. Wananchi wamebaki na shida kubwa. Ningependa Mhe. Rais aweze kuangalia haswa watu waliohamishwa kwa lazima na LAPSET. Vilevile tunayo barabara itokayo Lamu hadi Southern Sudan, inayoendelea kujengwa. Pia naomba wananchi walioko pale wawezekufidiwa ile maisha yao yaweze kuimarika na kuendelea inavyostahili. Nashukuru Mhe. Rais kwa hotuba yake. Aliweza kuguzia pesa za ‘Hustlers’"
}