GET /api/v0.1/hansard/entries/1201441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201441,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201441/?format=api",
"text_counter": 521,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "‘ Hustlers’ ni wengi sana katika Jamhuri ya Kenya. Nimeona ametenga jumla ya shilingi bilioni 50. Wasiwasi wangu ni vile hawa ‘ hustlers’ watakavyotambulika. Kusije kukawa kunao watu wengine ambao wasiostahili kufaidika na hizo pesa wakifaidika. Inafaa tuwe na utaratibu ambao utatusaidia kujua watu ambao watafaidika zaidi na huo mgao wa ‘ Hustlers’ Fund.’ Pesa hizo zitakapogawanywa katika kaunti zetu 47 za Jamhuri ya Kenya kuna mambo muhimu yanayofaa kuzingatiwa. Watu wafanyazo biashara ndogo ndogo kama vile mama mboga, vinyozi na akina mama wa salon wanafaa waangaziwe zaidi. Hatutaki kuona pesa hizo zikkifaidi mabwenyenye ambao wako na uwezo. Wasije wakachukua pesa zote, na wanaostahili wabaki bila mgao wowote katika zile pesa zinazonuiwa kuwasaidia. Bw. Spika wa Muda, jambo lingine ni ulipaji wa ushuru. Ushuru ni jambo ambalo lazima tuliangalie sana ili tuweze kulinda watu ambao wanahitaji kujiendeleza kibiashara. Ushuru wanaotozwa ni mkubwa sana. Hawawezi kujimudu kibiashara na kulipa huo ushuru. Ningependa sana hili jambo liangaliwe ili wananchi wafaidike. Itakuwa vizuri tukitengeneza sheria zitakazosaidia walipa ushuru kujiendeleza kibiashara. Isiwe kwamba wanalipa ushuru hadi biashara zao zinafifia, kufikia kiwango cha kutoweza kujiendeleza tena kimaisha. Bw.Spika wa Muda, nikimalizia, niko na imani na hili Bunge la Seneti, lenye jukumu la kulinda magatuzi yetu 47. Ninawaomba viongozi waliyotutangulia ama seniorleaders, waendeshe Bunge hili kwa njia inayostahili. Tuzingatie kwamba kuna viongozi waliotangulia na wale waliokuja baadaye, kama sisi wapya hapa. Watushike mkono vizuri ili watuelekeze. Vilevile tushirikiane na kusaidiana, ikizingatiwa ya kwamba sote tuko hapa kwa sababu ya kulenga halimashauri ya watu wetu. Bw. Spika wa Muda, itakapofika kwa ugavi wa rasilimali kwa magatuzi, tuone ya kwamba ugavi huo unafanywa kwa njia inayostahili. Hivyo ndivyo jinsi tutalinda magatuzi yetu na yaweze kuendelea kama vile Katiba inavyosema. Tumekuja hapa kuwakilisha watu wetu."
}