GET /api/v0.1/hansard/entries/1201468/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201468,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201468/?format=api",
"text_counter": 548,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili kuchangia kuhusu hotuba iliyotolewa na Rais William Samoei Ruto ambaye pia ni Kinara wa chama cha UDA. Nitaanza kwa kumshukuru Rais kwa kuniteua kama Seneta ili niweze kutoa mchango wangu. Asanteni Wakenya kwa kunipa fursa kama mtoto wa kike. Nilizaliwa na kulelewa katika mtaa wa Buxton kule Mombasa ambako kulikuwa na mradi wa affordable housing . Nilifurahi sana Rais aliposema kuwa Serikali yake itaanzisha miradi ya kujenga nyumba ili Wakenya wawe na makao bora. Mradi huo ulipoanzishwa kule Buxton, kulikuwa na hatihati na ambeambe nyingi. Hatimaye tuliukubali na kuukumbatia. Japo hakuna mwanadamu ambaye hukubali mageuzi kwa haraka, wakaazi wa Buxton walikubali kuhamishwa. Walipewa pesa kidogo za kuwakimu kwa muda wakisubiri nyumba hizo kujengwa. Kadiri muda ulivyoendelea, watu wa Buxton, mimi nikiwa mmoja wao, waliingiwa na hofu. Hatukuwa na uhakika kama tungepewa nyumba hizo. Kufikia sasa, wakazi wa Buxton hawajafanikiwa kupata tenant purchase scheme. Ombi langu kama mwakilishi wa upande wa Serikali ni hili. Ningependa sisi sote tulioko katika Serikali na wenzangu katika Upinzani tuangazie malalamishi ya wakazi waliondolewa pale. Tunafaa kuweka tofauti zetu kando ili miradi kama hiyo iyopendekezwa na Serikali ifaulu. Nakubaliana na Rais kwamba nyumba za Buxton hazikuwa za hadhi. Kwa hivyo, binadamu yeyote hakustahili kuishi pale. Nyumba hizo zilikuwa zinavuja wakati mvua ikinyesha. Ilimlazimu mtu kuweka vitu kama vijiko ili kuzuia maji ya mvua kulowesha nyumba. Waliokuwa wanaishi sehemu za chini walikuwa wanaathirika na vyoo vilivyojaa. Nyumba hizo hazikuwa za hadhi. Mimi kama aliyekuwa mkazi wa Buxton, kuna hofu miongoni wa waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo. Wana hofu kwamba Serikali inaweza kupeana ardhi hiyo kwa wawekezaji binafsi na kutotimiza malengo. Kwa hivyo, wale wanokusudiwa kufaidi mradi huo huenda wasifaidi. Ningependa Maseneta wanisikilize mimi kama muathiriwa. Natarajia wenzangu wafaidi. Tunafaa kupitisha sheria kwamba wale waliokuwa wanaishi kwenye nyumba hizo wanafaa kupata tenant purchase scheme, ili warudi katika nyumba zile. Jambo la pili, mimi natoka upande wa ukanda wa pwani. Namshukuru sana Rais kwa kuregesha huduma za bandari kule pwani, maana bandari ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu. Kwa Kimombo tunasema, the ecosystem of the economy of Mombasa andthe Coast at large. Namshukuru na kumpongeza sana. Hotuba ya Rais ilikuwa fupi. Namsihi Rais asisahau mradi wa barabara ya Dongo Kundu ambao utawezesha uchumi wa eneo la pwani kuimarika. Barabara ya Dongo Kundu imekuwa ikizungumziwa sana na Serikali. Kuna migao ya fedha mara tatu katika miradi ya Serikali."
}