GET /api/v0.1/hansard/entries/1201470/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201470,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201470/?format=api",
"text_counter": 550,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Taasisi ya bandari imekubali kwamba iliwahi kupokea fedha hizo. Jambo la kushangaza hadi leo ni kuwa wale waliokuwa wameondolewa katika ardhi pale Dongo Kundu, hawajawahi kufidiwa. Tungependa kujua tatizo liko upande gani katika taasisi husika. Pili, tuko na viwanda na rasilimali nyingi pwani. Kama alivyotangulia kusema ndugu yangu, Sen. Faki, kwamba utalii ni miongoni mwa uchumi wa pwani. Amezungumzia maswala ya open skies . Nitazungumzia ni wapi hasa Kenya iliadhirika upande utalii. Kenya iliadhirika zaidi wakati we privatized air ticketing of the tourismsector. Bw. Spika wa muda, kuna wakati hoteli zetu zote na destination zetu zilikuwa na vijumba kule ughaibuni, wakipiga ngoma. Na walipokuwa wakipiga zile ngoma, watalii wakipita wanavutiwa na utamaduni wetu kule nje. Ndiposa wanakata tikiti wanakuja kutembea. Siku hizi tunaambiwa kwamba we live in a digital era kwa hivyo watu wakate tikiti kupitia picha tu wanazoziona kwenye mitandao. Ningependekaza kama itawezekana, turejeshe hivi vijumba kule nje ili tupate watalii ndio uchumi wetu uweze kuimarika zaidi. Mwisho bila kusahau, ningependa kusisitiza Wakenya wawekeze ili tuache kuomba pesa ambazo tunatozwa riba kubwa sana ambayo inagandamiza ama kuujumu maendeleo ya nji yetu. Kuwekeza ni kujiwezesha. Hata hizi fununu zinazoendelea baada ya Raisi kuzungumzia kuhusu uwekezaji kwenye NSSF, hakuna ushuru ambao Raisi amependekeza. Amependekeza tuongeze akiba zetu ili tunapostaafu tupate pesa ambazo zitatustawisha katika maisha yetu ya uzeeni. Kwa hayo mengi ama machache, nawashukuru watu wa Mombasa kwa kunipa fursa hii, mimi mtoto wa kike, niweze kuwawakilisha katika Bunge hili."
}