GET /api/v0.1/hansard/entries/1201471/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201471,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201471/?format=api",
"text_counter": 551,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, jina langu ni Sen. Munyi Mundigi, chama changu ni Democratic Party (DP) kilichoko kwa mrengo wa Kenya Kwanza, kutoka Kaunti ya Embu. Pole kwa sababu nimechelewa kidogo. Embu kulikuwa na shida kwa inayotokana na wale watu wa familia moja waliochomwa na moto na tulikuwa tunawazika leo. Nilitoka hapa asubuhi, nikaenda Embu huko Runyenjes na nimerudi nikiwa nimechelewa. Ninaunga mkono mazungumzo ya Raisi, Mhe. William Ruto. Mazunguzo yake yalikuwa matamu kama asali ya nyuki. Pia yalikuwa mazuri kama ya mtu mwenye hekima kama mfalme aliyekuwa anaitwa Solomon. Kwanza, tangu tuchaguliwe hatujakaa siku nyingi ila tumeona matunda mazuri katika jimbo la letu la Embu. Kwa kipindi cha miaka 10 kulikuwa na vita, kutengana na kukosana na imeleta shida huko Embu. Watu walikuwa wanaenda kotini hapa na pale. Lakini wakati tumechaguliwa wakati huu, kumekuwa hakuna vita kwa sababu Rais alisema tuwe na amani na umoja. Hiyo ni sababu moja in ayonifanya nimuunge mkono. Pili, hosipitali zetu zote kwa muda wa miaka mingi zimekaa bila dawa. Ilikuwa ukienda hosipitali, ni kama unaenda kwa kifo. Lakini kwa muda wa siku chache, hosipitali zote ndogo na kubwa ziko na dawa. Aligusia pia mambo ya hela ya walipa ushuru. Kutoka siku hiyo, kama Serikali yetu ya Kenya Kwanza pamoja na ya kaunti ilikuwa inapata ushuru wa Kshs7 million sasa hivi wanapata mara tatu. Kwa hiyo, tunaendelea vizuri."
}