GET /api/v0.1/hansard/entries/1201899/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201899,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201899/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Nafikiria ni jukumu ndani ya Bunge hili la Seneti, kwamba upande huu wa walio wachache, watakuwa wakiiangalia Serikali inavyotekeleza wajibu wake. Ikiwa Serikali itatekeleza wajibu wake sawasawa, tutawapa kongole. Serikali isipotekeleza wajibu wake sawasawa, ni jukumu la upande huu kuikashifu na kuwaelekeza njia nzuri. Kazi ya upande huu isije ikawa inaingiliwa zaidi kutokana na sababu ya hoja za nidhamu zinazotoka upande wa Serikali. Ama pengine hawataki upande wa Upinzani uweze kuendelea na Hoja hii. Kwa nini upande huu hauna hoja nyingi za nidhamu kama upande wa walio wengi? Kwa nini ni mtu mmoja anazua hoja nyingi za nidhamu? Bw. Spika, ikiwa utaniruhusu, naweza kuchangia Hoja hii. Jambo la kwanza ni kukushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Kenya aliyoitoa katika kikao cha pamoja katika Bunge la Kitaifa. Mhe. Rais aliweza kuwapa Maspika wa Bunge la Kitaifa na Seneti kongole kwa kuchaguliwa kwao na vile vile Bunge hizi mbili zilikubaliana na uamuzi huo. Mhe. Rais alikuja Bunge wakati huo kutoa hotuba yake kama inavyoruhusiwa na Katiba. Jana, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Kenya aliweza kuingi katika majengo ya Bunge, bila Wabunge wowote kujua. Hakutoa taarifa yoyote kwamba angezuru majengo ya"
}