GET /api/v0.1/hansard/entries/1201923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1201923,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201923/?format=api",
    "text_counter": 177,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Spika, asante kwa kunikosoa. Hata hivyo, Mhe. Rais sio mtu wa kawaida bali ni Mhe. Raisi wa Jamuhuri ya Kenya. Bw. Spika, tunajua ya kwamba mahakama ni mahali ambapo kila mtu anaweza kwenda. Pia Bunge la Kitaifa ni mahali ambapo mtu yeyote anaweza kuja. Kulingana na uamuzi ulioufanya sasa hivi, pia katika wakati Bunge letu linafunguliwa kirasmi, ni taratibu za Bunge kuwaalika watu. Moja wapo ya waalikwa ilikuwa Mahakama Kuu ya Kenya. Iliongozwa hapa na Jaji Mkuu, Makamu wa Jaji Mkuu na Majaji wengine. Jambo la kushangaza ni kwamba sisi sote tunazingatia kwamba mikono ya Serikali ni mitatu. Katika hii mikono mitatu, ni upande ule wa utawala wa Executive, upande wa Bunge ambayo ni Legislature na upande wa Judiciary . Jambo lingine la kushangaza zaidi ni kwamba katika historia ya nchi yetu ya Kenya tangu enzi ya ukoloni, tukio hili halijatokea. Jaji Mkuu anaongoza Majaji wengine kuingia katika maeneo ya Bunge, kupiga msitari na kumngoja Mhe. Raisi. Tukio kama hilo halijawahitokea katika histroia ya Bunge na nchi hii. Tuliona kitendo hicho kuwa cha ajabu. Katiba inatuambia kila moja ya mikono mitatu ya Serikali, inaweza kujitetea na kujiangalia jinsi wanavyoendesha Serikali. Jambo lingine ni hili janga la njaa. Tunaona kuna mikakati tofautitofauti ambayo imefanywa na Mhe. Rais. Hata hivyo, kuna sehemu zingine ambazo zimekumbwa sana na janga la njaa. Baadhi ya sehemu hizi ni upande wa Turkana, Kaskazini mwa nchi, yaani Northern Frontier, kuanzia Mandera, Wajir, kuja mpaka Garissa. Vilevile maeneo ya Kilifi, Tana River, Kwale na Ukambani. Kila mahali kuna janga la njaa na mifugo ya Wakenya inamalizika. Ng'ombe na mbuzi ambao ndio chakula cha kutegemewa na wafugaji katika maeneo mengi wakufa njaa."
}