GET /api/v0.1/hansard/entries/1201925/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201925,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201925/?format=api",
"text_counter": 179,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Mhe. Rais katika Hotuba yake hakuangalia njia mwafaka ya Serikali kutatua janga la ukame na njaa. Hakueleza ni jambo gani ambalo Serikali yake itafanyia wafugaji ambao mifugo yao yanamalizwa na janga la njaa. Ninatoka katika maeneo ninayoyafahamu sana. Maeneo kama ya Ganze na Magarini yameathiriwa vibaya sana na janga la njaa na ukame. Kuna sehemu zingine nchini ambazo ni afadhali lakini zingine ukame umezidi sana. Bw. Spika, Mhe. Rais hakusema atasaidia hao Wakenya kwa njia gani ilihali hao ni Wakenya na walipiga kura. Wengine walimpigia kura na wengine hawakumpigia lakini wote walipiga ni Wakenya. Ni jukumu la Serikali kusaidia Wakenya walioathirika na janga la njaa na ukame. Hawa wenzetu wanapoteza mifugo wao na hawana chakula kwa sababu chakula hakiwezi kupandwa kule kikamea. Juzi walisema kwamba mbolea ya bei nafuu imepelekwa kila mahali. Hatukatai kwamba Serikali ilileta mbolea. Hata hivyo, utapata hii mbolea haijafika katika sehemu zingine. Sen. Mungatana alikubali hapa ya kwamba hajaiona hiyo mbolea kule upande wa Kaunti ya Tana River."
}