GET /api/v0.1/hansard/entries/1201927/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1201927,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1201927/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Mhe. Rais alisema kuwa watu wanaofanya kazi za kawaida kama wale wanaofanya kazi ndogo ndogo pia wanaweza kuwa na hazina inayowekwa kwa ajili yao. Hii ikimaanisha kuwa watu wawekeze kwenye National Social Security Fund (NSSF) ambayo ni shirika la wafanyikazi. NSSF ni shirika huru ambayo haliambatani. Wafanyikazi wenyewe wanasimamia shirika hilo. Mhe. Rais alisema ya kwamba ana mikakati ya kuanzisha mpangilio mwingine ambao unaweza kuangalia swala la pesa za wafanyikazi. Hii itakuwa kuingilia hali ya wafanyikazi na pahali ambapo wanaweka pesa zao. Itakuwa vyema kama hao wafanyikazi wataachiliwa wafanye kazi vile wanataka, waweke pesa zao wanapotaka hata kama itakuwa ni NSSF ilhali iwe ni jukumu yao. Katika hotuba yake, Mhe. Rais alisema ya kwamba ataaingilia kati na kupendekeza pesa zaidi kuwekwa katika NSSF. Hilo silo jambo nzuri. Kulingana na sheria za United Nations Charter, pesa hizi zinapaswa kuwa huru na Serikali haitakikani kuingilia katika matumizi yake ya kidemokrasia. Mhe. Rais aliposhika hatamu ya uongozi alisema amemsamehe yule aliyemkosea na aliomba wale waliokosewa na mtu yeyote kuwasamehe. Wakenya huangalia mbele wala si nyuma. Ni jambo la kusikitisha kuona ya kwamba baada ya Mhe. Rais kutamka maneno hayo sasa anajaribu kuingilia hazina ya wafanyikazi katika NSSF . Mhe. Rais akae kando na aache kuingilia pesa za wafanyikazi. Yule mkubwa wa hazina la NSSF na kiongozi wa wafanyikazi hawakuelewana naye kisiasa. Kiongozi wa wafanyikazi alijitoa na hayuko tena katika hilo shirika la hazina za kuweka pesa za wafanyikazi. Kwa hivyo, Mhe. Rais asiharibu wala asiingilie shirika hilo. Aliache shirika hilo liendelee katika hali yake ya kawaida."
}