GET /api/v0.1/hansard/entries/1202207/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1202207,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1202207/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Mheshimiwa Spika. Nachukua fursa hii kukupongeza kwa kuchaguliwa kama Spika wa Bunge na vile vile Mhe. Gladys Boss kama Naibu wako. Vile vile, nachukua fursa hii kuwashukuru sana watu wangu wa Jomvu kwa kunichagua niwe katika Bunge hili kwa muhula wa tatu. Haikua kazi rahisi; na kama wanavyoniita kule mtaani, “Kijana mwepesi, Garang Di Mabior na Mzee Fula Ngenge”, nawaambia kuwa niko hapa kwa nguvu za Mungu. Nitawahudumia kama vile nilivyowahudumia vipindi viwili vilivyopita. Vile vile, natoa pongezi kubwa sana kwa watu wa Mombasa kwa kumchagua mwenzetu tuliyekuwa naye hapa Bungeni, Mhe. Abdullswamad Sheriff Nassir, kuwa Gavana wa Jiji la Mombasa. Wakati wa Bunge la Kumi na Mbili, nilimweleza Mhe. Muturi aliyekuwa Spika wetu kuwa kama Mbunge wa Jomvu, sikuwa na wazimu nikisema Mhe. Abdullswamad angekuwa Gavana. Kwa hivyo leo, juu ya uongozi wako, twashukuru Mungu kwa kuwa Gavana wa Mombasa ni Mhe. Abdullswamad Nassir. Nikirejea Hotuba ya Rais, ilikuwa nzuri, fupi na haikuwa ya kuchosha. Alisema mambo mengi, mojawapo ikiwa ni jambo la CDF. Katika Hotuba yake katika kipengele cha 49, alizungumzia maneno ya CDF. Alisema kuwa imeweza kuleta mabadiliko makubwa. Ninavyofahamu, CDF ina kitengo cha mazingira, bursary, michezo na vilevile miradi. Hivi sasa, wazazi wote katika maeneo bunge yetu, wote wanatusumbua kwa kauli ya karo. Ni muhimu sana Serikali iangalie hili jambo la CDF ione kama tutasubiri lipitishwe kikatiba. Tunaposubiri kuipitisha kikatiba, ni muhimu kama Serikali ingepatia mambo ya"
}