GET /api/v0.1/hansard/entries/1202210/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1202210,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1202210/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Rais katika kipengele cha 29 ya Hotuba yake amezungumzia juu ya mambo ya makaazi ama affordable housing na vile vile, watu kupata haki ya kuona namna gani wataweza kupata makao. Hili ni jambo muhimu kwa sababu tukiangalia jambo la hatimiliki, ni muhimu kuliangazia. Na tunamshukuru Rais ameweza kuliangalia. Kwa maana hiyo, watu wangu walioko Aladina, Bangladesh, Owino Uhuru, Vikobani na sehemu mbalimbali wataweza, ikiwa Serikali itatia maanani mambo haya yaliyosemwa, kupata hatimiliki za ardhi na waweze kujiendeleza kwa maisha yao. Katika kipengele cha 48 cha Hotuba, Rais amezungumzia juu ya mambo ya janga la ukame. Hili ni jambo muhimu lakini pia tunasema mara nyingi Serikali ikiangalia jambo hili la ukame katika kuwapatia watu vyakula na usaidizi mwingine, huangalia maeneo kadhaa na wakatuacha sisi watu wa Mombasa kuonekana kuwa tunajiweza. Lakini yafaa ieleweke kuwa ndani ya mji wa Mombasa, kuna watu katika vitongoji ambao hawajiwezi. Ni muhimu Serikali ikitangaza majanga kama haya pia waangazie sehemu hizo."
}