GET /api/v0.1/hansard/entries/1202213/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1202213,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1202213/?format=api",
    "text_counter": 104,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Jomvu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
    "speaker": null,
    "content": "baada ya ile sumu ya Lead ambayo iliweza kuwapata watu hao. Waliambiwa walipwe pesa hizo. Katika Bunge ya 12, tuliyaleta maneno pale ambapo Mhe. Justin Muturi aliyekuwa Spika alituma Hoja hii kwa Mwanasheria Mkuu. Nakusihi Mhe. Spika, katika Bunge la 13, litume tena jambo hili kwa Mwanasheria Mkuu ambaye ni yule yule Justin Muturi. Itakuwa rahisi kwake yeye kuwalipa watu wangu wa Jomvu na hapo itaonekana “Fula Ngenge” kweli ameweza kufanya kazi kwa watu wake. Leo tuna matatizo mengi sana. Nikiangalia hali ya fidia, watu wengi walifutwa kazi katika Kenya Ports Authority (KPA) na jambo hili Gavana wetu wa Mombasa alipokuwa hapa akiwa Mjumbe wa Mvita, aliweza kulileta na tukaweza kuliunga mkono. Watu wale tungependa Serikali ione kuwa wamerejelea kazi katika sehemu ile ili waweze kukimu maisha yao. Vile vile, twampongeza Rais kwa kurudisha utendakazi wa Bandari katika mji wa Mombasa. Hili ni jambo ambalo tulikuwa tukilitamani kwa muda mrefu na leo tunampongeza kwa kufanya jambo hilo. Nataka kusema katika miji yote ambayo inaongozwa na iko na bandari, kwa mfano Antwerp, Long Beach kule Marekani, Durban kule Afrika Kusini kwenye Manispaa inayoitwa eThekwini, hao watu hupata pesa kutokana na hizo bandari. Kwa hivyo, ni hamu yetu tukiwa watu wa Mombasa kuona kuwa maadamu Bandari hii iko ndani ya Mombasa, tutaweza vile vile kuwa na kipato katika Bandari ya Mombasa. Lakini la zaidi, namshukuru Rais kwa yale ambayo ameweza kuyaangazia; kukupongeza na pia kuwapongeza watu wa Jomvu kwa kutuchagua, na wenzangu wote, kwa mara ya tatu. Ahsante Mheshimiwa Spika na Mwenyezi Mungu atubariki."
}