GET /api/v0.1/hansard/entries/1202353/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1202353,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1202353/?format=api",
    "text_counter": 244,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": null,
    "content": " Shukrani sana, Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Ningependa kwanza kutangulia kwa kutoa shukrani zangu zote za dhati kwa Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunipatia fursa ya siku hii ya leo; na vile vile kuweza kutoa shukrani zangu kwa wakaazi wa Nyali kwa kunichagua kwa mara ya pili licha ya changamoto ambazo tuliweza kuzipitia wakati wa uchaguzi mkuu uliopita. Wakati huo, asasi za usalama hususan viongozi wa asasi za usalama, walitumika vibaya sana katika Kaunti ya Mombasa kujaribu kubadilisha maamuzi ya wakaazi wa kaunti hiyo. Nataka kusema kuwa ushindi huu ni ushindi mara tatu kwangu binafsi. Ushindi wa kwanza ni ule wa kuchaguliwa kama Mbunge wa UDA nikiwa peke yangu katika Kaunti ya Mombasa. Ushindi wa pili ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Kenya kwa wana Mombasa kuweza kutoa asilimia arobaini na nne na kumchagua Rais wa wananchi, William Samoei Ruto. Ushindi wa tatu, ni ushindi wa Rais kuregeshea watu wa Pwani Bandari ya Pwani."
}