GET /api/v0.1/hansard/entries/1202356/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1202356,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1202356/?format=api",
"text_counter": 247,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": "nje bali tuwe tunafuata mfano wa nchi kama Uchina ambapo serikali inakopa katika asasi za serikali ndani ya taifa hilo. Pia, Rais alizungumzia Bunge la kazi. Alitaka Bunge hili lishirikiane na Serikali kuu ili tulete mabadiliko kwa mpigo na kuwahudumia Wakenya, hususan baada ya kupewa taifa lililobakwa, demokrasia kuharibiwa, mali kufujwa na waliofanya hivyo kuondoka kama wamemwachia Rais nchi uchi. Vile ambavyo amewachiwa nchi hii kwa hakika ni vile ambavyo hayati Emilio Mwai Kibaki aliwachiwa nchi hapo awali, kabla ya kuwaomba Wakenya wampe muda ile aweze kuboresha uchumi wa taifa hili. Alipopewa muda huo, bila shaka aliweza kufanya hivyo. Rais William Ruto amejipata katika mwanya huo huo, lakini kutokana na utendakazi wake, bidii, kutolala na kutopumzika, ameonyesha ishara tosha kwamba anaweza kuleta mabadiliko ya haraka na kuikwamua taifa hili. Kuna baadhi ya Wabunge ambao wamezungumzia Hotuba ya Rais, and kusema kwamba haikutaja maswala ya ufisadi. Tunataka kuwakumbusha kwamba hatuna wakati wa kutaja ufisadi kwa sababu tunajua wafisadi ni kina nani. Kazi ya Rais wa Jamhuri ya Kenya ni kuhakikisha kwamba wale wote waliofuja pesa za wananchi watashughulikiwa, na kuhakikisha kwamba pesa hizo zimeregeshwa kwa Wakenya. Ningelipenda pia kuzungumzia suala ya Hustler’s Fund – kile kitita cha pesa kilichowekwa. Hilo ni jambo ambalo amekuwa akitembea nchi nzima na kulizungumzia. Ni jambo ambalo litawafikia kina mama mboga, watu wa bodaboda na watu wa mkokoteni ili kuwasaidia, kwa sababu ile ya National Government – Constituencies Development Fund (NG- CDF) haitoshi na ina mipaka ya utumizi. Hotuba ya Rais iligusia pia maswala ya Mawaziri kufika katika Bunge hili la Taifa, na kuulizwa maswala nyeti kuhusiana na sehemu zao na Wabunge ambao ni waakilishi wa wananchi. Ni wazo zuri zaidi, na mapendekezo hayo ya kubadilisha na kuhakikisha kwamba Mawaziri hao wamefika yatakuwa mambo ya muhimu sana. Ikilinganishwa na Bunge la Kumi na Mbili, Mawaziri walikuwa wanajipiga kifua sana, na kujiona kama mungu-binadamu ambao hawawezi kuulizwa maswali wakati wanafanya makosa au wakati kuna dhulma katika taifa hili. Tunataka hadhi na heshima ya Bunge hili irejee kama zamani ili tuweze kuuliza maswali. Pia suala la NG-CDF limekuwa likizungumuziwa. Kama Mbunge wa Nyali, nimerudi hapa katika Bunge hili kwa sababu wa utumizi bora wa pesa za NG-CDF. Kuna hata magavana ambao wako na mabilioni ya pesa, lakini yale ambayo Wabunge wanafanya ni makubwa hata kushinda yale ambao hao magavana wanafanya. Pendekezo la kutoa pesa kwa Bunge la Seneti ni jambo zuri zaidi ili wapate nguvu za kusimamia na kuchunguza utumizi wa fedha katika kaunti mbalimbali. Mwisho, maswala ya makaazi aliyoyazungumzia ni bora zaidi, na bei ambayo imetolewa hakika mwananchi ataweza kulipa. Katika kipindi cha miaka fulani, mwananchi atakuwa na nyumba na sio kuishi katika mabanda kama mkimbizi wa ndani kwa ndani. Hatimaye, nina ujumbe kwa Wabunge wenzangu na wananchi pale nje wanaosubiri kwa hamu na ghamu kuona yale ambayo Rais atafanya. Nataka kuwaambia kwamba mtoto hazaliwi na akaanza kula chapati. Mtoto anazaliwa, ananyonya, anatambaa, anatembea kisha anaanza kula. Kwa hivyo, tuko katika sehemu ambayo Rais anapaswa apewe muda wake aanze kufanya kazi taratibu, akishirikiana na Bunge la Taifa, Bunge la Seneti na serikali za kaunti ili tuhakikishe kwamba tumekwamua taifa hili mahali ambapo tumewachwa. Yangu ni hayo tu, Mheshimiwa Naibu Spika. Pia nataka kutoa kongole na kukupongeza wewe binafsi na Mheshimiwa Spika kwa kuchaguliwa. Tunatumai mtatuongoza katika njia salama, na kuhakikisha kwamba sheria zinazotungwa ni za wananchi wa Jamhuri ya Kenya. Asante sana na Mungu awabariki Wakenya wote."
}