GET /api/v0.1/hansard/entries/1202647/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1202647,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1202647/?format=api",
    "text_counter": 68,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante Bw. Naibu wa Spika. Kwanza ninawapa kongole wanafunzi wote wanaofanya kazi katika hili Bunge la Seneti. Wako katika hali ya kujifunza jinsi kazi inafanywa ili watakapomaliza masomo, wawe wafanyakazi wa kutekeleza majukumu yao. Ninakubaliana na ndugu yangu, Sen. Mungatana, kuwa ingekuwa vyema kuona wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali ya taifa la Kenya. Tusiwatoe tu kaunti moja peke yake. Ni jambo muhimu kuwa Bunge la Seneti linatoa fursa kwa wanafunzi, waje kujionea viongozi wao wakiwa kazini. Watakapotoka hapa, watakuwa na elimu ya kutosha ambayo itawasaidia maishani. Vilevile, ni vizuri hili Bunge la Seneti lionyeshe mfano bora. Ni muhimu na pia ni jukumu letu sisi viongozi, kuonyesha njia murwa kwa watakaokuja baada yetu. Ninawashukuru Maseneta wenzangu kwa sababu wanakutana na hao vijana mara kwa mara na kupata maoni kutoka kwao. Tutaendelea kutembea pamoja nao na kuwafunza. Wakitoka hapa, niko na hakika elimu hii itawasaidia katika siku zijazo."
}