GET /api/v0.1/hansard/entries/1203484/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1203484,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1203484/?format=api",
    "text_counter": 401,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ganze, PAA",
    "speaker_title": "Hon. Kenneth Tungule",
    "speaker": null,
    "content": " Ndio. Ninachukua nafasi hii kuwashukuru watu wa Eneo Bunge la Ganze kwa kuniamini na kunichagua kuwa Mbunge wao katika Bunge hili la Kumi na Tatu. Nimechaguliwa kwa chama cha PAA. Kusema kweli ninashangaa hii leo ninaposimama hapa kusikia kuwa Wabunge wa Chama cha Muungano wa Azimio One-Kenya wakisema chama cha PAA ni miongoni mwa vile vyama ambavyo viko katika muungano huo. Chama cha PAA kilitoka katika Chama cha Muungano wa Azimio One-Kenya Coalition Party tarehe 5 Mei, miezi mitatu kabla ya uchaguzi mkuu. Hii ilifanyika kwa sababu ndoa ya PAA na Azimio la Umoja One-Kenya ilikuwa na mizozano mingi. Wakati wa kampeni, chama cha Azimio la Umoja One-Kenya kilipozuru kule Pwani kule mashinani, kilikuwa hakiruhusu wanachama wa vyama vingine waweze kuungana katika mikutano yao. Walikuwa pia hawaruhusu posta za kampeni zichapishwe katika chama cha Azimio la Umoja One-Kenya. Kwa hivyo, tulikuwa na shida wakati wa kampeni na wanachama wa Azimio la Umoja One-Kenya walikuwa na kiburi na madharau. Nashangaa kwa nini wanatutaka sasa ila hawakututaka wakati huo. Swali ninalojiuliza ni iwapo Azimio la Umoja One-Kenya wangeongoza serikalini wangekubali vyama vingine viwaunge? Tunashukuru Muungano wa Kenya Kwanza uliotukaribisha na tukafanya kampeni miezi mitatu kabla ya uchaguzi pamoja nao. Ninathibitisha kuwa wanachama wote wa Bunge la 13 wa chama cha PAA walio ndani ya Bunge hili hawako katika Muungano wa Azimio la Umoja One- Kenya na wako katika Muungano wa Kenya Kwanza. Hapo ndipo tutakapokua katika muda wa maisha ya Bunge hili. Asante sana, Mheshimiwa Spika."
}