GET /api/v0.1/hansard/entries/1203672/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1203672,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1203672/?format=api",
    "text_counter": 125,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika, asante sana. Kitu cha kwanza umesema ya kwamba lazima mtu abonyeze kidole ili uweze kuona katika kile kioo chako ulicho nacho hapo mbele. Utaweza kuona ni nani amefinya kibonyezo cha hoja ya nidhamu. Bw. Spika, katika Bunge hili, ni kawaida ya kwamba upande ya walio wachache na walio wengi, mtu yeyote anaweza kubonyeza kidole. Lakini, kwa mara ya kwanza, ninaona ya kwamba huyu ndugu yangu Sen. Olekina alikuwa amebonyeza kidole cha komputa lakini pengine wewe umeona ama pengine umefinya jicho lako moja hukuweza kuiona."
}