GET /api/v0.1/hansard/entries/1203764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1203764,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1203764/?format=api",
"text_counter": 217,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa ya kuchangia katika swala hili la hoja ya nidhamu. Katika nchi yetu ya Kenya, tumebahatika kuwa na sheria tofauti ambazo zinahusiana na ndoa. Tunaweza kulinganisha maswala yanayomkumba Sen. Ali Roba na wenzake hivi sasa, na ndoa katika jamii. Ndoa ya Kiislamu inampa fursa mwanamume kuoa wake zaidi ya mmoja. Unaweza kuoa hata mpaka wa nne. Lakini ndoa ambayo hufungwa kwa Msajili wa Ndoa, huwa ni mke mmoja na mume mmoja. Mkataba uliofanyika chini ya sheria ya Political Parties, ambao tuliufanyia marekebisho Januari mwaka huu, hapa katika Bunge hili la Seneti, hairuhusu chama kuwa katika coalition mbili wakati mmoja. Sen. Ali Roba amesema hapa kwamba, tayari wameshapeleka kesi mahakamani kuomba mkataba uvunjwe. Ushaskia hayo? Wako mahakamani wakitaka mkataba wao na Azimio-One Kenya Coalition Party ubatilishwe. Kabla ya hayo kuamuliwa, bado wao wako katika Azimio-One Kenya Coalition Party. Sisi tunakuhesabu kama mwana Azimio-One Kenya Coalition Party."
}