GET /api/v0.1/hansard/entries/1204054/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1204054,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1204054/?format=api",
"text_counter": 507,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, Kamati inayobuniwa ni muhimu kwa Bunge la Seneti. Ni Kamati ambayo itatoa mwongozo kwa kazi yote inayoendeshwa katika Bunge hili. Kwa hivyo, hatuwezi kupuuza hii Kamati. Kama Bunge la Seneti na ikiwa hili ndilo swala letu la kwanza ambalo liko mbele yetu, ni lazima tufuate sheria kulingana na Katiba na Kanuni zetu za Bunge la Seneti. Tumeona kwamba baadhi ya majina yaliyopendekezwa yameleta utata. Utata ni kwamba; je, Sen. Ali Roba amependekezwa na upande wa walio wengi ama upande wa walio wachache? Mheshimiwa Spika, swala la ni nani walio wengi au wachache katika Bunge hili ni swali ambalo litatatuliwa kutokana na mwongozo utakaotoka kwa mkurugenzi wa vyama vya kisiasa. Mambo mengi yamezungumziwa hapa. Swala ni je chama cha United Democratic Movement (UDM) kiko katika mrengo gani katika Bunge hili? Mpaka sasa, mwongozo uliotoka kwa mkurugenzi wa vyama vya kisiasa ni kuwa chama cha UDM bado kiko katika mrengo wa Azimio-One Kenya Coalition. Hili swala hata Sen. Ali Roba mwenyewe amelizungumzia akasema kuwa tumepeleka kesi mahakamani na mahakama bado haijatoa mwongozo. Kwa hiyo---"
}