GET /api/v0.1/hansard/entries/1208073/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1208073,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1208073/?format=api",
"text_counter": 61,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kuria East, UDA",
"speaker_title": "Hon. Maisori Kemero",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Mhe. Naibu wa Spika kwa kunipa nafasi hii. Ninaomba nichukue nafasi hii kutoa rambirambi zangu kwa familia ya mwendazake na vile vile kwa watoto wake. Siku nyingi watu wengi hawatambui kwamba kwa sababu wazazi wao hutekeleza majukumu ya kitaifa, watoto hawa hubaki bila kushughulikiwa kama vile watoto wengine wa kawaida. Vile vile, ninatoa rambirambi zangu kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa imebainika hapa kuwa marehemu Mhe. Githunguri alizaliwa Tanzania na baadaye akarudi nyumbani na kuweza kutenda makuu tuliyosikia hapa. Pole kwa familia, kwa watu wa Kiambaa na kwa Wakenya wote kwa jumla. Kwa niaba ya wakaazi wa Kuria, nasema pole kwa majirani wetu kutoka Tanzania kwa sababu wao pia wameshiriki katika msiba huu. Mwenyezi Mungu aweze kutusaidia sote kwa sababu uongozi huambatana na kujitolea. Marehemu Mhe. Stanley alijitolea na ametutangulia. Wacha Mungu azidi kuitwa Mungu. Ahsante sana."
}