GET /api/v0.1/hansard/entries/1208159/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1208159,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1208159/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Matuga, ANC",
    "speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
    "speaker": null,
    "content": "sahihi utekelezaji wa miradi ya mali ya umma. Wasitie sahihi tu wakisema mradi ni wa Umma! Sharti wajue kwamba wao pia ni wahusika. Na endapo hiyo miradi haitafanyika vizuri basi wao binafsi.... Nafikiri kungekuwepo na mwongozo kwamba ikiwa mtu ana sign kama Waziri ama mhandisi, a sign mara mbili. Kwanza ana sign kiofisi na pili yeye mwenyewe anaelewa na kuridhika kuwa mradi ule utafanyika kwa wakati unaofaa na rasilimali zitatumika vyema. Huwa haingii akilini kwamba mradi unaweza kutiwa sahihi na mkandarasi kutoka nje, kwa mfano, Uchina ilhali bado haujafanyiwa tathmini kuwa utaanza lini. Katika eneo Bunge langu la Matuga tumekuwa na mradi wa maji. Umetiwa sahihi, mkandarasi amekuja, ameweka mali yake pale na pia vyongozi wa serikali wamekuja kuuzindua. Lakini kuna mgogoro baina ya Wizara inayohusika ya Maji na Wizara ya Misitu. Wizara ya Misitu haijatoa idhini kwamba mradi ule ufanyike lini lakini tayari sahihi zishatiwa. Ninavyo fahamu kama mweledi wa nyanja hii, kuna kipengele kinachosema kwamba mradi tu nimetia sign, kuna pesa italipwa kabla ya mkandarasi kuanza kazi. Na isipolipwa basi itagharimu riba ndani yake. Mara nyingine unapata kwamba kwa sababu mradi umechelewa, ile riba ambayo mkandarasi anadai hata inazidi ile pesa ambayo angekuwa analipwa kufanya hii kazi. Hivi sasa kuna mradi tunaita Dongo Kundu kule eneo la pwani. Mkandarasi amefanya kazi kufikia asilimia 94; imebaki tu asili sita. Ingawa hivyo anadai fedha ambazo amepeana cheti kwa muda wa zaidi miezi sita sasa. Kulingana na mkataba kuna riba mle ndani kwa sababu hajalipwa kwa wakati unaofaa. Riba inazidi ile pesa anayo dai. Tusisahau kwamba anadai pesa hii kwa kiwango cha sarafu ya kigeni ambayo ni ya dola. Saa hizi, ukiangalia ubadilishaji wa pesa kati ya dola na shilingi za Kenya tunazungumzia mabilioni ya shilingi za Kenya kama deni. Lakini anadai pesa ya kigeni na deni inazidi kuongezeka. Kwa hivyo, nikimalizia kuunga mkono Hoja hii, wale wanaotia sahihi pia wanastahili kuwajibika kibinafsi. Wasifikirie hii ni pesa ambayo haina mwenyewe ilhali ni pesa ambayo kila mwananchi, hata yule wa chini, amechangia. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii."
}