GET /api/v0.1/hansard/entries/1208347/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1208347,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1208347/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante Bw. Spika. Naunga mkono ndugu yangu, Kiongozi wa Walio Wengi, alivyosema kwamba kuna njia panda; tukilinganisha njia ya Kamati ya Bunge nzima ama sivyo, tuchague Kamati. Tulikuwa tushaongea hapo awali, mimi na yeye na tukakubaliana kwamba njia ya Kamati maalum ndio itakuwa njia mwafaka sana. Njia ya Kamati teule itawapa nafasi wale Maseneta watakaochaguliwa nafasi ya kuipa Seneti njia au mwelekeo kulingana na zile karatasi zote ama stakabadhi zitakazokuwa zimeletwa katika kusikiliza kesi hii. Sio rahisi mtu kuletwa Seneti na haki yake ionekane kupotoshwa. Wale Maseneta tutakuwa tumechagua kuhudumu katika Kamati maalum wafanye kazi mwafaka, ambayo wataangalia zile stakabadhi zote na wazikague, waone ni wapi ambapo watapitia na kutuambia hii ndio njia ya kisawasawa. Vile vile, tukiifanya yote kwa njia ya Kamati ya Seneti Nzima, itakuwa ni muda mdogo sana ambapo tunaweza kuchukua nafasi hiyo kukubaliana ama ripoti kuwa ile itaweza kuchambua yale mashtaka na yule atavyokuwa amejitetea ili kuweza kuja na mwelekeo fulani ambao utaweza kuangalia ni njia gani utaweza kupitia. Kwa maoni yangu, njia ile ya Kamati Maalum ndio njia ambayo itaweza kufafanua na kubaini kama huyo Gavana ni kweli alifanya yale anayodaiwa ama hakufanya. Pili, sisi Maseneta tuna imani na ile Kamati ambayo tutachagua. Tunajua ya kwamba Maseneta wote walioko hapa wana uwezo wa kuhudumu katika Kamati Maalum. Lakini, kuna sababu zake muhimu ndani ya sheria ni kwa sababu gani tunasema ya kwamba watu wakiwa kama 11, sio kama watu ambao wako zaidi ya 60. Kwa hiyo, wale watu 11 wakikaa katika Kamati Maalum, watakuwa na wakati maalum wa kupitia zile rekodi itakuwa bora zaidi kuliko sisi tukitumia Kamati ya Seneti Nzima ama Committee of the Whole House."
}