GET /api/v0.1/hansard/entries/1208349/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1208349,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1208349/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Nina imani na Kamati Maalum itakayo chaguliwa. Tuko na imani ya kwamba watatupatia mwelekeo wa kisawasawa. Vile vile, tumekuwa hapa ndani ya Seneti na ni wakati za kuthibitisha ya kwamba Seneti, vile tunavyosema ndio ‘nyumba kubwa’ ya Bunge hili letu la Kenya. Kwa hivyo, tuchukue nafasi hii kuona ya kwamba haki imetendeka kwa mshtaki na mshtakiwa. Mshtakiwa pia apewe nafasi nzuri ya kuangalia stakabadhi atakazojitetea, ili tuone haki iko upande gani. Kwa maoni yangu, ninahimiza Maseneta wenzangu tuende njia ya Kamati kwa sababu hiyo ndiyo njia ambayo itatupatia uamuzi kamili."
}