GET /api/v0.1/hansard/entries/1208501/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1208501,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1208501/?format=api",
    "text_counter": 276,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kuchagua Kamati Maalumu ya kuchunguza madai yaliyoletwa katika Seneti hii na Bunge la Kaunti ya Meru. Kifungu cha 80(1) ya Kanuni za Kudumu zetu kinasema kwamba Seneti inaweza kwenda kwa njia ya Kamati ya Seneti Nzima ama kwa njia ya Kamati Maalumu ya kuweza kuchunguza madai haya. Kuna kile tunaita umuhimu katika njia zote mbili katika kuchunguza suala hili. Mpaka sasa, nafikiri yaliyoletwa mbele ya Seneti hii ni madai tu. Wakati Seneti Nzima au Kamati itakapokaa, ndiyo ule ushahidi wa kuthibithisha madai yale utafikishwa mbele ya Kamati ile ama Seneti Nzima ili kuweza kuamua kama kweli mashataka yana uzito ama hayana. Si kweli kwamba Seneti hii siyo mahakama. Sasa, itakaa kama mahakama kuweza kuchunguza ukweli wa madai ambayo yamewasiliswa na Bunge la Kaunti ya Meru. Bw. Spika, kuna uzito kuhusiana na madai ambayo yameletwa, kwamba jinsia moja imepunjwa katika uteuzi wa Kamati hii. Kuna uzito fulani na hatuwezi kupuuza. Kwa kuwa hii ni Seneti mpya na ni mara ya kwanza suala kama hili linafika hapa, ipo haja ya Wabunge waweze kukaa na kukusikiza. Nimeona leo japo kuwa ni Kikao Maalumu tumeweza kupata karibu full House. Kila Seneta ameweza kuwacha kazi zake akaja katika Kikao hiki. Nina imani kwamba iwapo itafanywa kwamba ni Seneti Nzima ikae kusikiza madai haya, Seneti hili litaweza kuvunja kazi zao waweze kukaa hapa kusikiza kwanzia mwanzo mpaka mwisho ili uamuzi utolewe. Bw. Spika, ili kuwapa Maseneta wapya fursa ya kuangalia masuala kama haya, ingekuwa bora tuwe na Kamati ya Seneti Nzima kuchunguza suala hili sababu hii ndio kesi ya kwanza ya kuchunguza Magavana tunasikiza katika Bunge hili. Uamuzi utakaotoka, utakuwa funzo kwao ambao hawajapata fursa ya kuchunguza Magavana. Ile kesi itakayofuata inaweza ikafanywa katika njia ya Kamati Maalum lakini hii ya kwanza katika Bunge hili, itakuwa bora tuichunguza kama Kamati ya Seneti nzima ili kila Seneta apate fursa ya kusikiza kesi hii. Kuna wengine katika Bunge hili wamelala na hawajui kitu gani kinachoendelea. Kwa hivyo, dai kuwa baadhi ya Maseneta hawatakuwa na hamu ya kusikiza ushahidi katika Kamati ya Seneti nzima ni singizio la kukataa mfumo huo. Tunajua Kamati zetu nyingi za Seneti zikikaa kwa vikao vyao, ni wachache wanaochangia masuala yaliyo mbele yao. Bw. Spika, hii haitakuwa mara ya kwanza kufanya hivyo. Naomba Hoja hii izingatiwe katika Kamati ya Seneti Nzima ili wale hawajapata somo kama hili wapate ujuzi au uzoefu wa masuala kama haya. Bw. Spika, asante kwa kunipa fursa hii."
}