GET /api/v0.1/hansard/entries/1208611/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1208611,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1208611/?format=api",
"text_counter": 386,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "wa uchaguzi uliyopita. Lakini baada ya haya masuala yote kuangaliwa na Kamati teule, sisi kama Bunge tutakuja hapa tuyajadili na tuwe na msimamo wetu. Tuna jukumu lingine, tutapata fursa ya kuangalia ikiwa hii Kamati yenyewe itaona kuna dosari fulani, ama kuna shutuma moja ambayo wameona ni mbaya. Nina hakika tukiwa na Sen. Sifuna ambaye najua ni mzoefu wa mambo ya kisheria, ninaona kuna vijana kama vile Oketch na Kamau. Sijui ni kwa nini Maseneta wote hawajaridhika na kuunda kwa Kamati hii. Wengine wanasema ya kwamba ile impeachment ikifanywa katika Seneti Nzima tutajua vile masuala dhidi ya Gavana yalivyoendelezwa. Hakuna jambo linafanywa katika Seneti au Kamati bila kunukuliwa. Hawa ndugu zetu wataandika yote ambayo yatajadiliwa katika Kamati hiyo. Hawa Maseneta ni wasomi. Mimi najua wataweza kusoma na kujua jambo la kufanya. Watasoma hata zaidi. Jambo ambalo limenishtua sana ni kwamba Seneta wa Busia, Sen. Okiya Omtata anataka kuleta matata. Ameleta mambo mengine mapya ambayo yanataka kutuelekeza kutuambia kwamba tusimamishe shughuli za Bunge tufanye mikutano ya Kamkunji na maandamano. Hatutaki mambo kama hayo siku ya leo. Tunamaliza hii shughuli leo. Pengine kama kutakuwa na Kamkunji ni baada ya masaa yaliyowekwa na Seneti hii. Lakini kutuambia tutoke kando tufanye hivyo, atakuwa akiongoza Seneti hii katika shughuli ambazo sisi hatujazizoea. Lakini namuelewa kwa sababu pengine sasa ndio anajifunza mambo ya Seneti. Amekuwa akishughulika katika korti na hata nimesikia akikuita Jaji, wewe Bw. Spika. Asante Bw. Spika."
}