GET /api/v0.1/hansard/entries/1208843/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1208843,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1208843/?format=api",
"text_counter": 43,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Kwanza, ninatoa kongole kwa ndugu yetu, mhe. David Wakoli Wafula, kwa kupata ushindi mkubwa na kuwa Seneta wa Kaunti ya Bungoma. Tuliona kile kindumbwendumbwe kilichokuwa huko. Ninawaunga mkono kwake kupata ushindi na ni jambo nzuri kuwa naye hapa. Nina uhakika atafanya kazi ya useneta kwa ustadi mkubwa. Aliyekuwa Seneta wa Kaunti ya Bungoma sasa ndiye Spika wa Bunge la Kitaifa. Seneta Wetangula alikuwa kiongozi wa Walio Wachache na alijithibitisha vilivyo kama mwakilishi wa kaunti hiyo. Vile vile, alikuwa kama taa katika hili Bunge la Seneti. Ni jambo nzuri kuwa Sen. David Wafula amekuja kujiunga nasi. Uhakika anavaa viatu vikubwa. Kwa hivyo, watu wa Bungoma wanatarajia kwamba atafanya kazi kama alivyofanya mhe. Wetangula. Ni jambo la furaha na tunamtakia kila la kheri. Jambo la muhimu ambalo Sen. David Wafula anapaswa kulielewa ni kwamba katika Bunge la Seneti tunajaribu tunavyoweza kuona kwamba mijadala yetu haiegemei upande wowote. Mijadala yetu huwa ni ya kitaifa. Yote tunayofanya hapa ni kusaidia serikali zetu za mashinani. Kwetu hilo ndilo jambo muhimu. Mimi nataka kumpa wosia kuwa awe mkakamavu kama sisi wenzake. Hata ikiwa kama alivyosema ndugu yangu mdogo Sen. Cherarkey ya kwamba akienda kwa induction ni sawa pia wengine wanaojisikia kwenda waandamane naye. Watafundishana wakiwa huko na hatimaye wakirudi watakuwa mabingwa ndani ya hii Seneti yetu. Namtakia kila la kheri ndugu yetu Sen. David Wafula katika kazi yake anayoeanza kuifanya leo. Nina hakika kwamba watu wa Bungoma hawakufanya makosa kumchagua yeye kama Seneta wao. Ndugu yangu, watu wako wana imani na wewe. Kwa hiyo, kuwa mkakamavu katika kazi yako. Kama kuna jambo lolote unaweza kuja kuuliza upande huu ambao umejaa maprofesa, huko huru kufanya hivyo. Upande ule mwingine hakuna maprofesa."
}