GET /api/v0.1/hansard/entries/1208895/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1208895,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1208895/?format=api",
    "text_counter": 95,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Mimi pia nilikuwa mwanachama wa chama cha Ford Kenya awali katika safari yangu ya siasa. Karibu katika Seneti. Tunatarajia mchango wako utasaidia pakubwa Bunge hili Pamoja na watu wa Kaunti ya Bungoma. Katika kura ambayo ulishiriki, kulikuwa na vyama vingi ambavyo viliweza kukupinga. Nafikiri kitu ambacho kilitushangaza ni kuwa wale wengine wanaokupongeza hivi sasa wako katika vile vyama ambavyo vilikuwa mstari wa mbele wakiponda chama chako na kukuponda wewe binafsi kama mgombea wa kiti cha Seneti katika Kaunti ya Bungoma. Hawakumpa heshima Spika wa Bunge la Kitaifa sasa, ambaye ni kiongozi wa chama cha Ford Kenya; kuwa pale ni nyumbani kwake na kwa hivyo angependa apate kijana kiongozi ambaye yeye mwenyewe ameweza kupendelea."
}