GET /api/v0.1/hansard/entries/1209059/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1209059,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209059/?format=api",
    "text_counter": 259,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante Bw. Spika. Kwanza, nataka kumpa kongole ndungu yangu, Sen. (Dr.) Khalwale, kwa kuongoza Kamati ilyochunguza mambo haya. Sote tunawapata hongera kwa kazi mlioifanya kama Kamati. Pili, nataka kumweleza dada yetu Gov. Kawira kwamba amepewa mamlaka na wananchi wa Kaunti ya Meru. Ni lazima uangalie mamlaka unayoyatumia na utendakazi wako kwa watu wa Meru ili wafurahie kwa sababu wamekuchagua kama kiongozi. Mambo ya kujipiga kifua na kusema kuwa wewe ndiye kila kitu pale tuiweke kando. Tenda kazi kwa watu wa Meru. Shirikiane pia. Huwezi kuwa kiongozi kama gavana kama hushirikiani na MCAs wako. Kushirikiana ndiko kutaleta maendelo na hayo ndio yanatakikana na watu wa Meru. Dada yangu, weka kibri, kujidai na vitu vyako vyote ambavyo vinafanya MCAs kutofanya kazi na wewe kando na utumikie watu wa Meru na kusaidia MCAs kuleta maendeleo katika maeneo yao. Huo ndio wasia wangu kwako. Umeponea chupu. Waswahili husema. Otherwise ungeiona barabara ya kuenda nyumbani."
}