GET /api/v0.1/hansard/entries/1209150/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1209150,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209150/?format=api",
    "text_counter": 350,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika unajua sisi hatujazaliwa na mama mmoja wala baba mmoja, pengine fikra zangu na vile ambayo ninaangalia maneno ni tofauti lakini kwa sababu tayari mimi ninakuheshimu na ume niambia niwachane kufuata huo msururu wa maneno nimewacha. Ningependa kumwambia Governor ya kwamba aungane na viongozi wale wengine waweze kufanya kazi pamoja. Waswahili wanasema “Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu”. Mkifanya kitu pamoja na mkiwa pamoja mtatembea mbali kwa sababu ukitaka kwenda mbali mweende mkiwa pamoja lakini ukitaka kwenda haraka uende peke yako na utasulubiwa ukiwa peke yako. Ahsante."
}