GET /api/v0.1/hansard/entries/1209155/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1209155,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209155/?format=api",
"text_counter": 355,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kathuri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13590,
"legal_name": "Murungi Kathuri",
"slug": "murungi-kathuri"
},
"content": "Bw. Spika, hii Kamati ya Ugatuzi inayoongozwa na mwenye kiti Sen. Abass, ningeomba ipige kambi Meru ili iweze kusaidia ugatuzi wa Meru. Waweze kujadiliana pia wawapee ushauri. Mheshimiwa Sen. Abass Mwenyekiti wa hii Kamati ni kiongozi ambaye tumefanya naye kazi katika Bunge la Kitaifa. Ninajua ushauri wake na Kamati yake utasaidia sana Gavana wetu na usaidie County Assembly ndipo tuweze kuendelea. Siku ya leo sio siku ya ushindi wa mtu mmoja, tuseme tukitoka hapa eti tumeshinda na hao wengine wameshindwa. Ningependa tutoke hapa kama Meru imeshinda kwa ujumla."
}