GET /api/v0.1/hansard/entries/1209510/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1209510,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209510/?format=api",
"text_counter": 345,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Ahsante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, nataka kupongeza Kamati hii kwa sababu wamefanya kazi nzuri wakiongozwa na Sen. (Dr.) Khalwale. Lakini kwa sababu sijasoma hii ripoti, kuna maswali niliyokuwa ninajiuliza. Kwanza kabisa hawa MCAs - madiwani wote ambao wako Kaunti ya Meru, wote walionekana kuegemea upande mmoja. Nilikuwa nikijiuliza hayo maswali kwani, ijapokuwa nimesikia ya kwamba Kamati waliongea nao na wakawaambia kwamba washikane na Governor ili waweze kuendelea mbele ni vizuri sisi tuweke sheria hapa kwa sababu kazi yetu ni kutunga sheria, itakuwa ni muda gani governor atakuwa nao ili aweze kuletwa hapa ili kutibuliwa. Jambo lingine ni kwamba Kamati ya hapa Seneti; Kamati ya Ugatizi imezembea katika kazi yake. Wanaweza wakakupatia sababu nyingi lakini ukweli wa mambo ni huu, wanapaswa kuwa wametembelea zile kaunti. Nilipokuwa mwenyekiti wa kamati ya ugatuzi, tulitembelea Kaunti ya Murang’a na mwenda zake Sen. Kabaka; Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Tukatembea Kisii. Tukaenda mpaka Taita Taveta na haya mambo hayangefika hiki kiwango ambacho kimefika. Jambo lingine ni kuwa Sen. Cherarkey alipokuwa hapa alisema ya kwamba vile ambavyo Kamati walivyofanya kazi, hawakufanya yeye mwenyewe alifikiria angefanya. Watu wote ambao wanasimama hapa kutoa heko kwa Kamati unasema hao wamefanya viziri, lakini Sen. Cherarkey alipo simama hapa kusema ameona mkushi katika hii Kamati vile walivyofanya maneno, mulimtimua---"
}