GET /api/v0.1/hansard/entries/1209518/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1209518,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209518/?format=api",
"text_counter": 353,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kathuri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13590,
"legal_name": "Murungi Kathuri",
"slug": "murungi-kathuri"
},
"content": "Ahsante sana Bw, Spika kwa fursa hii. Ninashukuru Bunge hili la Seneti kwa sababu ya kutoka kwa likizo yao ili wakuje hapa kwa hizo wiki mbili kuskiza maswala ambayo yako Meru. Hii ni siku kubwa sana ya Wameru nikiwa mmoja wao. Yale mambo yote ambayo yamejadiliwa katika Kamati ya wale Maseneta kumi ma moja, ni mambo yaliyokuwa wazi kwa Taifa nzima kwa sababu yalikuwa kwa rununu ama kwa teolevisheni zetu. Kwa sababu nimekuwa katika vikao vyote, wanakamati wameshauri viongozi wote; wameshauri Gavana wa Meru, walishauri pia MCAs wetu. Na kwa vile yale mawswala yako wazi kabisa katika vichwa vyetu tukiwa Wakenya, ningeomba Gavana wangu kwa sababu yuko hapa: Kwa sababu umepata fursa nyingine ya kuhudumia watu wa Meru nakuomba kwa unyenyekevu nikiwa Seneta wako pia uweze kuwafikia wale viongozi wa Bunge la Kaunti ya Meru, uweze kukaa nao chini haraka iwezekanavyo ndipo muweze kushauriana vile mtafanya kazi pamoja. Kenya hii imeangalia Meru kwa macho mawili, Meru imekuwa sasa ndio ile inatwa trending, inatrend kabisa katika taifa. Sisi tukiwa viongozi wale wamechaguliwa Meru, mimi Seneta na wale viongozi wengine, Members of Parliament (MPs) tutafanya vile tutaweza ili tuendeleze Meru pamoja. Wewe mwenyewe pale ulisema na unajua ile shida iko Meru na vile ungependa kufanya kazi yako. Tafadhali, ninaomba ukirudi Meru, enda ufanye vivyo hivyo. Kaa na wale viongozi wetu; sisi wote hatutahama Meru. Tumezaliwa pale Meru tutazikwa pale siku ile tutakufa. Kwa hivyo tuungane sote na tufanyie Wameru kazi."
}