GET /api/v0.1/hansard/entries/1209590/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1209590,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209590/?format=api",
"text_counter": 60,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kathuri",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13590,
"legal_name": "Murungi Kathuri",
"slug": "murungi-kathuri"
},
"content": "Bw. Spika, ninakushukuru sana kwa nafasi hii ili nimkaribishe rafiki yangu Seneta mpya ambaye amechaguliwa juzi, Sen. William Kisang. Tumefanya kazi na yeye miaka 10 katika Bunge la Taifa. Ninamjua kama kiongozi aliwafanyia watu wa eneo Bunge lake kazi nzuri sana. Ninachukua nafasi kuwapongeza wale wangeni walioko katika Bunge hili kutoka Kaunti ya Elgeyo Marakwet kwa sababu ya kumuuunga mkono na kumchagua mhe. Kisang kuwa Seneta wao. Sen. Kisang, ninakukaribisha katika Bunge hii kwa roho safi sana kwa sababu wewe ni rafiki yangu wa kindani. Kabla ya uchaguzi tuliongea tukiwa ziara fulani ya kikazi na nikakuambia kuwa mimi ninaenda Seneti nawe ukaenda ule upande mwingine. Ninashukuru Mungu kwa sababu ametuunganisha tena tuweze kuwafanyia Wakenya kazi. Nikiwa Naibu wa Spika hapa tutaungana na ninaomba uingie kwa kamati ile uliyokuwa unaipenda ya ICT na zingine ambazo utataka kufanyia kazi ili tuweze kutekeleza kazi yetu vizuri. Ninashukuru sana, Bw. Spika."
}