GET /api/v0.1/hansard/entries/1209637/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1209637,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209637/?format=api",
"text_counter": 107,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "(PSC) imeingia hapa na hiyo ndio tashwishi. Shirika hilo lisingefaa kuwa hapa. Ningependa kukubaliana na Kiongozi wa Waliowengi kwamba hiyo nambari ya PSC ingepewa Wabunge au vyama. Kwa hivyo, sioni kama kuna shida sana. Lakini sioni sababu ya PSC kuwekwa katika hiyo hesabu. Pili, tunaelewa ya kwamba katika hali ya uchaguzi nchini yetu, Kenya, kunakuwa na shida kubwa sana. Watu huwa na ukabila na utengano kwa sababu ya kura. Lakini ikiwa watu wa dini wanaweza kupewa nafasi hizo ili wawe na nafasi ya kuchagua mume na mke mmoja, itakuwa jukumu lao kuwaleta kwenye jopo ambalo litachagua makameshina. Mwisho, ni lazima tuzingatie uhuru wa IEBC. Kwa sababu, mara nyingi tunaona ya kwamba inaweza kuingiliwa na kuwa na upotevu fulani. Aliyekuwa Mwenyekiti wa IEBC, Bw. Chebukati, alisema kwamba aliweza kutendewa vitu fulani ambavyo avikuwa na ushahidi wa kutosha. Lakini ikiwa kutakuwa na vitu kama hivyo, basi kutakuwa na umuhimu sana kuona ya kwamba shirika ambalo linasimamia uchaguzi nchini liwe uhuru sana. Lisiwe huru kidogo ili waweze kuingiliwa au kuambiwa kitu fulani basi, liwe huru zaidi. Kwa hivyo, maoni yangu ni hii ndio njia ya kwenda. Ninaunga mkona Hoja hii."
}