GET /api/v0.1/hansard/entries/1209708/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1209708,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209708/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ninasimama kuunga mkono na kusema ya kwamba ni viziri vile hili Jopo la Uteuzi limeundwa. Nikiangalia naona ya kwamba vile liko ni vizuri kabisa. Ukweli wa mambo ni kwamba wakati wote sheria ambayo inahusu uchaguzi inaposhughulikiwa, kumekuwa na vurugu na mvutano lakini kwa wakati huu nina furaha kwa sababu tutaongea kwa amani bila vurugu ya kuelewana kwa sababu sharia hizi za uchaguzi zinahusu Wakenya wote. Nimesikia Sen. Osotsi akisema ya kwamba kuna wale ambao hawapaswi kuwa wakiangaliwa zaidi, wale wanaopaswa kuangaliwa ni vyama. Ninataka kumwambia ya kwamba watu wote wana sehemu katika uchaguzi kwa sababu uchaguzi si wa wanasiasa peke. Wakati wa kupiga kura hata wale ambao ni watu wa kanisa na wafanya kazi wa umma wana jukumu la kupiga kura na kufanya uamuzi. Ni vizuri kila mtu ahusishwe. Ninasimama kuunga mkono na kusema kuwa hii sehemu moja ambayo imepatiwa hawa ambao ni wa Tume ya Utumishi wa Umma, wale wabaki pale kwa sababu wanajua mambo ya kisheria. Hasa nikisema kuhusu"
}