GET /api/v0.1/hansard/entries/1209710/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1209710,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209710/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": ", wale ndio watakaoshughulikia zaidi. Nimesikiliza ndugu zangu wakisema ya kwamba hii ni sehemu ya serikali. Watumishi wa Umma wale ambao hautawaweka kwa serikali hii ama ile kwa sababu wanafanya na serikali iliyoko na ijapokuwa nilisikia ati wanapoteuliwa na rais ni mpaka waletwe katika Bunge. Bunge lenyewe lina usemi; wanaweza kukataa ama kukubali. Kwa hivyo, Bunge lina usemi katika sehemu ile. Vile ambavyo imetengenezwa kusema ya kwamba kuwe na watu katika Tume ya Bunge; mwanamume na mwanamke mmoja, ninaunga mkono mia kwa mia. Vile vile, watumishi wa umma ni mpaka washughulikiwe. Mahali ambapo nina tashwishi ni hawa wanasheria. Kila mahali kukitajwa katika serikali ama katika sheria unapata ni mpaka hawa wanasheria watajwe ama ile tume ya wanasheria. Swali ni hili : kuna wale ambao ni madaktari na wahandisi. Hata hao wanapaswa kushughulikiwa. Ninaona Sen. Omogeni akisema mpaka waangaliwe kwa sababu yeye ni mwanasheria. Ninaona Sen. Madzayo pia akisema mpaka waangaliwe lakini Sen. Thang’wa hapa si mwanasheria naye ataangaliwa wakati gani ? Ni vizuri hata badala ya kusema watu wa kutoka Law Society of Kenya (LSK) waangaliwe wangesema mwanasheria tuu ili hata wao waweze kuangaliwa. Wale ambao ni wachungaji ama religious organizations - nimesikia wengine wakisema ati ni mpaka tuzingatie na tuseme ati mmoja awe ni Mwislamu na yule mwingine awe ni Mkristo lakini hakuna haja ya kusema hayo yote kwa sababu wenyewe wanajua vile ambavyo wanapaswa kufanya. Mimi nitafuatilia haya na ninaunga mkono kwa sababu sheria hizi ndizo zitakazosaidia tukiendelea mbele---"
}