GET /api/v0.1/hansard/entries/1209911/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1209911,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209911/?format=api",
    "text_counter": 103,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Mwenyekiti wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nikiangalia marekebisho yaliyoletwa na Sen. Mumma, ninapatwa na shida, yeye kusema ya kwamba katika Jopo la Uteuzi angependa kumwondoa mwakilishi wa Tume ya Utumishi wa Umma. Ningemwomba kwa unyenyekevu aweze kuondoa hayo marekebisho kwa sababu mwakilishi wa Tume ya Utumishi wa Umma ni muhimu zaidi wakati hii Tume inapofanya kazi yake. Vile ambavyo mwenyekiti wa kamati ambayo walikuwa wakifanya kazi wakiwa pamoja, Sen. Wakili Sigei, ameweza kuondoa marekebisho aliyoyaleta, bila marekebisho, vile ilivyotoka katika Bunge la Kitaifa hivyo ndivyo inafaa zaidi. Kwa hivyo, ningemwomba Sen. Mumma akubali kuondoa hayo marekebisho ili tupige kura bila ya kujaribu kuondoa mwakilishi huyu wa kamati ya Utumishi wa Umma kwa sababu inafaa zaidi tuwe na mwakilishi pale. Nimemsikia Seneta wa Kaunti ya Nairobi akisema kwamba siasa ni mtazamo. Ikiwa siasa ni mtazamo, itaonekana aje wawakilishi wa Tume ya Umma hawana mwakilishi yeyote? Hata pale kutakuwa na shida; itaonekana kwamba hata sisi hatuwatambui wafanyikazi wa umma. Yeye mwenyewe alisema kuwa ni mtazamo wa kisiasa na vile vile wale wafanyikazi wa umma ni Wakenya na wanapaswa kuwa na usemi wakati ile tume inapoundwa. Asante, Bw. Mwenyekiti wa Muda."
}