GET /api/v0.1/hansard/entries/1209977/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1209977,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1209977/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Mwenyekiti wa Muda, kwa nafasi hii ambayo umenitunuku. Ni nafasi yangu ya kwanza kutaja au kuchangia pakubwa kuhusiana na swala la IEBC na mchakato mzima wa kikosi cha kuchagua watu hawa. Tume ya Serikali ambayo inahusishwa pakubwa kuajiri watu kazi ni lazima ipewe nafasi yake kikatiba ili iwape Wakenya watu ambao wana tajriba, wakakamavu, historia yao inaeleweka na wanaweza kuwajibika katika majukumu yao."
}