GET /api/v0.1/hansard/entries/1210005/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1210005,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1210005/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Mwenyekiti wa Muda. Naunga mkono mapendekezo ya Sen. Mumma. Ukweli wa mambo ni kuwa sisi sote ni binadamu. Sen. Wakili Sigei ambaye ni shupavu katika masuala ya sheria asubuhi alipendekeza marekebisho kwa Mswada huu. Hata hivyo, amerudi hapa alasiri na akageuza mwelekeo. Tumejipata katika njia panda. Nasema hivyo kwa sababu sisi hatuwezi kuwa conveyor belt ya Bunge la Taifa. Kama wao hawawezi kufanya kazi kisawasawa, sisi tutafanya kazi yetu kisawasawa. Kamati ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu inaheshimiwa sana hapa Seneti. Ripoti zinazotokana na Kamati hiyo ni muhimu kwani zinaongoza sheria tunazopitisha hapa Seneti. Kama tunavyojua kuna leo na kesho. Leo, unaweza kupitisha sheria inayokupendelea wewe na kesho sheria hiyo hiyo, ikukate wewe ukijipata upande huu mwingine. Wenzangu tuliokuwa nao katika Bunge la Kumi na Moja na Bunge la Kumi na Mbili watakumbuka kuwa kulikuwa na kiongozi hapa ambaye leo ninavaa viatu vyake aliyeitwa Sen. James Orengo ambaye alituonya kwamba tuwewaangalifu wakati tunajadili na kupitisha sheria hapa Seneti. Tusijetukapitisha sheria ambazo zitatukimbiza kwa ofisi yake tukitaka utetezi. Naona tutajipata katika hali aliyotabiri mhe. Orengo kama tutapitisha Mswada huu jinsi ulivyo. Sen. Wakili Sigei, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu alitueleza vizuri sana katika kikao cha asubuhi lakini sasa amegeuka kama kinyonga ambaye hugeuka rangi mara kwa mara na kuwa kitu kingine. Lazima tuwewaaminifu ili wananchi wanaotutazama waelewe kazi yetu hapa Seneti. Hatufai tuonekane kuwa sisi ni mikanda tu ya kubeba mizigo kutoka Bunge la Taifa Naunga mkono mapendekezo ya Sen. Mumma kwa sababu Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za Kibinadamu ameshindwa kueleza kinaga ubaga na kutushawishi ni kwa sababu gani amekubaliana na mapendekezo ya Bunge la Taifa na kutupilia mbali mapendekezo yake aliyoyaleta hapa Seneti wakati wa kikao cha asubuhi."
}