GET /api/v0.1/hansard/entries/1210013/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1210013,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1210013/?format=api",
    "text_counter": 205,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Mwenyekiti wa Muda, ninaunga mkono mapendekezo ya Sen. Mumma kwani makamishna wa tume ya utumishi wa umma wanachaguliwa na Mhe. Rais. Hivyo, Mhe. Rais atakuwa na uwezo mkubwa juu ya tume hiyo. Sisemi kuwa Mhe. Rais atatumia mamalaka yake vibaya. Leo Mhe. Rais anaweza kuwa mzuri na kutumia sheria hiyo vizuri. Je, kesho tukipata Mhe. Rais mwingine? Tukiwa hapa kama Wabunge ni lazima tupitishe sheria ambazo zitawafaidi watoto wetu, wajukuu wetu and vitukuu wetu. Siku moja wakija hapa, waweze kusema ya kwamba, ‘wazee wetu ambao walikuwa hapa kama Sen. (Dr.) Khalwale walipitisha sheria ambayo ilidumu maisha.’ Naunga mkono mapendekezo ya Sen. Mumma kwa sababu yanaleta mwelekeo na uelekezi wa Bunge la Seneti."
}