GET /api/v0.1/hansard/entries/1210048/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1210048,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1210048/?format=api",
    "text_counter": 240,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sifuna",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13599,
        "legal_name": "Sifuna Edwin Watenya",
        "slug": "sifuna-edwin-watenya"
    },
    "content": "Bw. Mwenyekiti wa Muda, unanijua kama mtu wa heshima kwa wale wote ambao wanakalia kiti hicho. Hata hivyo, haiwezekani, kwa mfano, Sen. Methu kusema kwamba anaona pembe kwenye kichwa cha Sifuna na isemekane kwamba hatuwezi kuzungumzia hilo. Ikiwa ulinisikia vizuri, nilianza kwa kusema sijui nifanyeje mimi kama Seneta wakati ambapo wewe ukiwa kwenye kiti hicho unatoa hoja ambayo kwangu mimi ni uongo wa wazi kwa sababu nina macho. Nilikuwa nimechanganyikiwa na sikujua cha kufanya mimi kama Seneta."
}