GET /api/v0.1/hansard/entries/1210266/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1210266,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1210266/?format=api",
    "text_counter": 45,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Mr. Speaker, Sir, Ugandans speak fluent Kiswahili. We have been to their Parliament . Kiswahili kitukuzwe. Bw. Spika, ninawashukuru ndugu zetu kutoka Uganda. Natumai wanaelewa tunapoongea Kiswahili. Tunawafurahia kama wageni wetu wa Bunge la Seneti. Najua waliokuja ni Waandishi wa Taarifa Rasmi ya Bunge. Niko na Imani kwamba, waliyoyaona katika Bunge la Seneti, yanadhihirisha kwamba hili ndilo Bunge la juu Kenya. Tukiwa hapa, sisi huwa na mijadala tofauti. Najua nyinyi kazi yenu ni ya kuweka rekodi za Bunge kisawasawa. Niko na imani kwamba, mtabeba yale mazuri mnayojifunza na kuona hapa na kwenda kuyaendeleza katika Bunge lenu. Tumewafurahia sana kwa sababu mmekuja katika nchi yetu. Mumekaribisha sana hapa Seneti. Ninawaomba msimalizie shughuli zenu hapa Nairobi. Mkipata nafasi, kuna mandhari mazuri hapa nchini ambapo mnaweza kuzuru na kujionea, kwa mfano, kule Mombasa na Kilifi. Pia mnaweza kuzuru mbuga la wanyama la Maasai Mara wanapoishi Wamaasai. Pia tuna Samburu National Park na sehemu zingine. Mkitembea sehemu zote za Kenya mtaona vile Wakenya wanavyoishi. Mumekaribishwa sana Kenya, hasa katika Bunge la Seneti. Asante, Bw. Spika."
}