GET /api/v0.1/hansard/entries/1210404/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1210404,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1210404/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Spika, hatupingi uamuzi uliotoa kwamba Sen. Sifuna atoke nje kwa sababu amejibizana nawe. Ningependa kusema kitu kimoja. Aliyeanzisha fujo hakutolewa licha yake kufanya hivyo mara mbili akiwa hapa ndani. Alitoka pale alipokuwa ameketi akaja hapa na kusema alivyosema na ukamwambia aketi lakini hakukaa. Ulipoendelea kuongea, alirudi hapa mara ya pili na akaendelea kujibizana nawe. Amejibizana na upande huu kwa mara ya tatu kwa sababu alikuwa anamwambia asikilize amri ya Spika. Kama wangekuwa wachezaji wa mpira, basi wote wawili walifanya makosa. Ukipeana kadi nyekundu huku, unafaa kupeana kule pia ili wote wawili watoke nje. Hiyo itaonyesha kuwa haki imetendeka. Sipingi uamuzi uliofanya. Hata hivyo, kuna yule aliyeanzisha fujo mpaka yule Seneta akatolewa nje. Hatufai kuwa na ubaguzi wa aina yoyote."
}