GET /api/v0.1/hansard/entries/1210470/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1210470,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1210470/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante Bw. Spika. Naunga mkono yote yaliyosemwa na ndugu yangu kiongozi wa walio wengi, Sen. Cheruiyot. Kwanza, nawashukuru maseneta ambao wako hapa sasa hivi. Wale saba ambao wako kwenye list hii ni maseneta ambao wamechaguliwa na upande ule mwingine na upande huu wa walio wachache pia. Nikiangalia hii list ya hawa maseneta saba, ni watu waliojukumika, walio na taaluma tofauti tofauti ambazo wataleta katika Senate Business Committee (SBC). Nataka kuwapatia kongole kwamba ni watu ambao wamekamilika kisawa sawa. Kuna Sen. Ali Roba, aliyekua gavana. Dadangu Sen. Veronica Maina ni wakili mkubwa. Ndugu yangu Sen. Wakili Segei ni wakili mkubwa. Dadangu Sen. Tabithe Keroche ni mtu mwenye taaluma kubwa sana ndani ya nchi yetu ya Kenya. Mamangu, Sen. Kavindu Muthama, pia ni mmoja wa wale wenye taaluma ya juu sana. Sen. Faki ni wakili mkubwa naye Sen. Sifuna akiwa pia ni mmoja wa mawakili waliojitambulisha juu sana hapa Kenya. Sen. Sifuna alikua ni mwandishi mkuu katika chama cha Orange Democratic Movement (ODM) na utendakazi wake ulikuwa wa hali ya juu sana. Nampongeza vile vile kwa kuja katika kamati hii ya SBC. Vilevile yeye husema ukweli lakini hasira zikizidi ni kama za binadamu. Kuna samaki mmoja kwenye maji anayeitwa mkizi. Wanasema hasira za mkizi saa zingine inakuwa furaha kwa mvuvi. Lakini hapa, Sen. Sifuna amejitambulisha kama seneta mshupavu. Jukumu letu---"
}