GET /api/v0.1/hansard/entries/1210795/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1210795,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1210795/?format=api",
    "text_counter": 189,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kingi",
    "speaker_title": "The Speaker",
    "speaker": null,
    "content": " Sen. Abdul Haji and Hon. Senators, maybe I will switch to Kiswahili, so that we may make progress. Waheshimiwa Maseneta, ninawasihi tusome Kanuni za Kudumu zinazoendesha ratiba ya Bunge la Seneti. Tukifanya hivyo, shughuli yetu ya Bunge itakuwa rahisi sana. Bunge hili liko na sheria zake. Hata tupitie shida aina gani, shida hiyo iko na sheria zake ambazo zimewekwa wazi hapa. Nimewasikiliza wale waliosimama kwa hoja za nidhamu na nikasema nitatoa uamuzi wangu. Pia nikasema ikiwa una jambo ambalo linahusu lile swala ambalo tayari tumeshazungumzia katika hoja zenu za nidhamu, hakuna haja kusimama na kulizungumzia tena. Sen. Abdul Haji, unayoyazungumza ni yale ambayo tumeshazungumza. Kwa hivyo, umekiuka nidhamu. Tafadhali, mambo ya barua iliyoandikwa na Kiongozi wa Walio wachache nimeyazungumzia hapa. Mambo ya barua ambayo Sen. Abdul Haji amezungumzia, pia iko mezani mwangu. Wakati ninatoa uamuzi, hayo yote tutayaweka bayana na hatutachelewa. Ni kweli kwamba upande wa Walio Wachache wanasema kuwa wako na hamu ya kwamba tulitatue jambo hili na twende mbele. Mimi ninawahakikishia upande wa Walio Wachache, kwamba kamwe sitachukua muda kutatua jambo hili. Uamuzi wangu utakuja kwa haraka na sidhani kwamba tutachelewesha haki yenu. Kwa hivyo, tafadhali mada hii ambayo tumeshaizungumzia tuiwache pale kisha mnipatie fursa ili nilete uamuzi. Na mimi sitauchelewesha uamuzi wangu. Asanteni."
}